• Mawasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Baruapepe za Watumishi |
    • Malalamiko |
GAIRO DISTRICT COUNCIL
GAIRO DISTRICT COUNCIL

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Gairo

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo
    • Idara
      • Utawala na Rasilimali watu
      • Maendeleo ya Jamii
      • Mipango, Takwimu na Ufuatiliaji
      • Maji
      • Ujenzi na Zima Moto
      • Kilimo, Ushirika na Umwagiliaji
      • Aridhi na Maliasili
      • Usafi na Mazingira
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Mifugo
      • Afya na Ustawi wa jamii
      • Fedha na Baishara
    • Vitengo
      • Teknolojia, Habari na Mawasiliano.
      • Kitengo cha Manunuzi
      • Sheria
      • Mkaguzi wa ndani
      • Uchaguzi
      • Ufugaji wa nyuki
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
    • Kilimo
    • Mifugo
  • Huduma Zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Leseni
    • Maji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Uvuvi
    • Huduma za Watumishi
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu za Halmashauri
    • Ratiba za Vikao
  • Miradi
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Ripoti
    • Sheria Ndogo
    • Fomu
    • Sheria
      • Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya 1977
      • Katiba inayopendekezwa
  • Kituo cha Habari
    • Maktaba ya Picha
    • Maktaba ya Video
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Hotuba

JABIRI MAKAME AIPONGEZA TBS KWA KUTOA MAFUNZO YA UDHIBITI WA SUMUKUVU KWENYE MAZAO

Posted on: December 2nd, 2021

Mkuu wa Wilaya ya Gairo Mhe. Jabiri Omari Makame amelishukuru na kulipongeza Shirika la Viwango Nchini (TBS) kwa kuendesha mafunzo kwa wadau wa kilimo Wilayani humo juu ya udhibiti wa Sumukukuvu kwenye nafaka hasa mahindi na karanga pamoja na bidhaa zake.

Makame ametoa pongezi hizo Disemba 2.2021 katika ufunguzi wa mafunzo ya siku tatu ya Udhibiti wa Sumukuvu kwa Wadau mbalimbali wa Kilimo Wilayani Gairo yanayo endeshwa na TBS kwa kushirikiana na Mradi wa TANIPAC uliopo chini ya Wizara ya Kilimo, katika kumbi za Diana, Msufini Pub na Ukumbi wa mikutano Hosipitali ya Wilaya ya Gairo.

“Ninaishukuru TBS kupitia mradi wa TANIPAC chini ya Wizara ya Kilimo kwa kutoa kipaumbele cha kuendesha mafunzo haya muhimu kwa Wananchi wa Gairo kuhusu elimu ya usalama wa chakula hususani katika udhibiti wa Sumukuvu kwenye Mahindi, Karanga pamoja na bidhaa zake”, alishukuru Mhe. Makame.

Makame alisema kuwa Gairo ni miongoni mwa Wilaya 18 nchini zinazotajwa kuwa na tatizo kubwa la Sumukuvu hali ambayo alisema inatishia usalama wa chakula na kuhatarisha afya ya Watumiaji wa nafaka hasa mahindi na karanga.

Alisema “Chakula kisicho salama husababisha madhara ya kiafya na vifo kwa walaji pamoja na athari nyingine za kiuchumi, hivyo ni wajibu wetu sote kuzingatia mikakati ya kukabiliana na changamoto ya Sumukuvu ili vyakula vyetu viendelee kuwa salama kwa muda wote”.

Naye Mwenyekiti wa Kamati ya kusimamia Mradi wa kudhibiti Sumukuvu TBS-TANIPAC Ndugu Jabiri Saleh Abdi alisema changamoto ya sumukuvu ni kubwa kwani inasababisha madhara kwa walaji na kwamba husababisha udumavu kwa watoto wadogo.

“Sumukuvu husababisha madhara makubwa kiafya kwa binadamu na Wanyama ikiwepo magonjwa ya kansa na vifo kwa binadamu, lakini pia hata huleta udumavu kwa watoto wetu kushindwa kuwa na ustawi mzuri katika ukuaji. Nahii ni kwa mujibu wa takwimu zilizotokana na tafiti mbalimbali zilizofanywa na Wizara ya Kilimo”, alifafanua Ndugu Abdi.

Uchafuzi wa sumukuvu unatajwa kuenea zaidi katika Mikoa 10 na Wilaya 18 nchini Tanzania ikiwemo Wilaya ya Gairo, ambapo TBS kupitia mradi wa kudhibiti sumukuvu TANIPAC umeanza kutoa mafunzo kwa Wakulima, Wafanya biashara za mazao, wasindikaji wa bidhaa zinazotokana na mahindi na karanga sambamba na wasafirishaji wa mazao kwa lengo la kuhakikisha changamoto hiyo inadhibitiwa kikamilifu.


Matangazo ya Kawaida

  • MAELEKEZO YA KUJIUNGA NA KIDATO CHA KWANZA 2022 SHULE ZA BWENI December 03, 2021
  • ORODHA YA WANAFUNZI WALICHAGULIWA KUJIUNGA KIDATO CHA KWANZA MWAKA 2021 December 18, 2020
  • FOMU ZA MAELEKEZO YA KUJIUNGA NA KIDATO CHA KWANZA SHULE ZA SEKONDARI GAIRO 2021 December 17, 2020
  • TANGAZO KWA WAAJIRIWA WAPYA-KARIBUNI WILAYA YA GAIRO July 01, 2021
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • ACHENI KUIBUA MIGOGORO NA WATENDAJI WENU,JENGENI MAHUSIANO MAZURI

    May 21, 2022
  • WATUMISHI 3, KATI YA 4 WAREJESHWA KAZINI, 1 ASIMAMISHWA KUPISHA UCHUNGUZI

    May 20, 2022
  • WADAU WA ELIMU GAIRO WAKUSANYA SH.38 MILIONI KATIKA HARAMBEE YA KUTUNISHA MFUKO WA ELIMU

    January 14, 2022
  • MADIWANI GAIRO WAIOMBA TARURA KUWABANA WAKANDARASI WANAOKWEPA KULIPA USHURU WA HUDDUMA

    January 11, 2022
  • Tazama zote

Video

TAZAMA FILAMU YA TANZANIA THE ROYAL TOUR
Video zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Zabuni za Manunuzi
  • Zabuni za Ujenzi
  • Huduma

Viunganishi Linganifu

  • Ikulu ya Tanzania
  • CHANEL YETU YA YOUTUBE
  • Utumishi
  • TAMISEMI
  • Ofisi ya Takwimu
  • Idara ya Habari Maelezo

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Mawasiliana nasi

    Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya Gairo-Mtaa wa Malimbika, Kata ya Gairo.

    Sanduku la Posta: 40, GAIRO

    Simu ya Mezani: +255232935454

    Simu ya Kiganjani: +255 767498981

    Barua pepe: ded@gairodc.go.tz, info@gairodc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Hakimiliki©2018 Halmashauri ya Wilaya ya Gairo. Haki Zote Zimehifadhiwa